The House of Favourite Newspapers

JPM Arejea Dar, Sasa Kuanza Ziara Zenji

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amerejea jijini Dar es Salamaa na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili akitokea mapumzikoni Chato mkoani Geita leo Alhamisi, Januari 9, 2020.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa, amesema kesho Ijumaa, Januari 10, Rais Magufuli ataanza ziara ya kikazi ya siku tano visiwani Zanzibar baada ya kutoka mapumzikoni nyumbani kwake, Chato mkoani Geita.

“Rais ataweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar, ataweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyopo Mjini Magharibi na atafungua hoteli yenye hadhi ya nyota tano, Hotel Verde Zanzibar – Azam Luxury Resort and Spa.”

Leave A Reply