The House of Favourite Newspapers

JPM ATOA TSH 50M KWA TAIFA STARS ‘MKIFUNGWA MTAZITAPIKA’- VIDEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amekutana na kuzungumza na wachejazi wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Ijumaa, Oktoba 19, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam na kuwapa pesa kiasi cha Tsh. Milioni 50 kwa ajili ya kuimarisha kambi yao.

Stars wako mbioni kwa ajili ya kwenda kuweka kambi kujiandaa na mchezo wao wa kufuzu Mashindano ya AFCON 2019, dhidi ya Lesotho mwezi ujao.

“Mimi siyo shabiki wa timu yoyote, kwa sababu kila timu ninayojaribu kuishabikia hapa nchini haifiki popote. Ni aibu sana nchi ina watu zaidi ya milioni 50 tunakosa watu 11 wa kufanya vizuri kwenye Timu ya Taifa, ndiyo maana Watanzania wengi wamekuwa wakishabikia timu za nje. Mimi nilicheza sana mpira nikiwa kidato cha kwanza na cha tatu nafasi ya forward, baadaye nikawa goal keeper, nilipoanza kuvaa miwani nikaacha kucheza mpira, kwa hiyo mimi ninapenda mpira. 

“Juzi nilikuwa kwenye hatua ya mwisho kutoa ndege, nikaambiwa uwanja ule hautoshi kutua ‘Dream Liner’, nilipoanza kufuatilia dakika za mwanzo mmeshapigwa mbili kavu, kipindi cha pili mkapewa na ‘dinner‘ ya tatu. Nikasema ni nafuu ndege yangu sikutoa, ninataka niwaambie ukweli, inasikitisha, nina uhakika machungu ninayoyapata Watanzania wengi wanayapata. 

“Tuliingia tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere, hatujaingia tena. Tumekuwa tukipongezana tu kwa vikombe vya hovyo hovyo, eti mnaitwa Bungeni wanawapa vichwa tu, ninawaambia ukweli. Hata viongozi wa michezo wamekuwa majizi, hata FIFA ilikataa hata kutupa fedha tulizoakiwa kupewa sababu ya matumizi mabaya, nilipoingia madarakani nikasema hata kama umekula rushwa kwenye michezo lakini utapelekww mahakamani tu.

“Mtu anahangaika sana kuomba nafasi, anahonga sana, akishapata nafasi anakwenda kukomba pesa tu. hata kwenye klabu zeu nako ni hivyo hivyo. Ikiwezekana katika viwanja vyote, muweke Electronic Ticketing, ili kudhibiti mapato na kuipatia mapato yake Serikali. Nilipoingia madarakani nilianza kufikiria kama timu zote hazifanikiwi labda nichague wanajeshi, kazi yao iwe mazoezi ya mpira tu kuanzia asubuhi mpaka jioni, na ndiyo niiwafanye iwe Timu ya Taifa, kipa akifungwa anawekwa ‘lokapu’, akitoka ni mpira tu.

“Sasa hivi Timu ya Taifa tunakwenda vizuri, hasa tulipopata huyu Kocha Emmanuel Amunike wa Nigeria, nikasema labda huyu kwa sabau ni mweusi atakuwa na machungu ya Uafrika. Tumefungwa bao tatu kavu, nyie mkapata bao mbili halafu mnasema mmeshinda? Bado! niliwashangaa hata waliokuwa wakisghangilia. Ndiyo maana nikasema ngoja niwaite leo nisikilize changamoto.

 

“Nimeambiwa mnataka kuingia kwenye mazoezi ili mshinde mechi yenu inayokuja, nimatumaini yangu mikienda huko mtashinda mechi zote, tumechoka Watanzania kuwa wasindikizaji, jina la nchi ni kubwa, lakini kila unapoenda mnafyatuliwa tu, ni aibu. Huu ni muda wa kubadilika, niwaombe wachezaji, sasa tuichukue hii kama vita, viongozi wa michezo msimuingilie kocha kumpangia kikosi, yeye ndiye anawafahamu wachezaji nani acheze wapi ili lawama wakati mwingine ziende kwake, vijana wajitume.

“Ukitaka kuwa mchezaji mzuri lazima uachane na pombe, ulevi, uachane na uhuni, utafunga magoli mengine lakini hili lingine hautafunga kwa sababu unakuwa umechoka, Nimeelezwa mnajiandaa kwenda Lesotho kwa ajili ya mazoezi, mimi nitawaongeza Tsh. Milioni 50, na hizi pesa ziwe kwa ajili nya watu wnaotakiwa kwenda tu, siyo wachezaji wanakwenda 16 halafu viongozi 30, kwa nini? Wengine wanajipa kazi useless.

“Nitashangaa sana watakaoenda Lesotho wachezaji 22 halafu wasindikazaji 40, viongozi wanakwenda kazi zao ni kulala mahotelini, wanajipa vyeo visivyofaa, tukiendelea hivi hatutafika mbali, naamini nyinyi mtatuvusha. Ndugu zangu ninawaambia sasa mmeingia kwenye mkataba wa ajabu, si mmekubali kuja hapa? Nitafuatilia hata senti tano kujua imeliwa wapi, na ole wao waile, siwezi kutoa Tsh. Milioni 50 ya walipa kodio halafu ikachezewa tu, nataa ikatumike kwa mazoezi.

“Wakati mwingine tusiwategemee sana wachezaji walioko nje, wanakuta wenzao wameshafanya mazoezi, kwa sababu tu ya majina yao wanalazimika kupangwa. lakini si vibaya kuwatumia kwa sababu Samatta pale ameingiza goli, wawe wanawahi kwenye mazoezi. 

 

“Niwaombe na wengine wanaoweza waichangie Stars, kila pesa itakayochangwa, Wizara ya Michezo na TFF lazima muwaelze wananchi mliitumiaje, wakati mwingine Watanzania wanachoka, huwezi kuchangia kilaza kila siku, lazima uchangie mtu anayeshinda. Hizi Tsh. Milioni 50 nilizowapa zikaleta ushindi, ninataka ushindi, ninawaeleza ukweli, mkishindwa mtazitapika kwa njia nyingine, tushinde tufike AFCON, Mungu awabariki sana!” amesema Rais Magufuli. 

VIDEO: MSIKIE HAPA JPM AKIZUNGUMZA

Comments are closed.