JPM Awatumbua DC na DED Nachingwea

Leo Jumamosi Oktoba 19, 2019 Rais Dkt. John Magufuli amefanya Uteuzi wa Viongozi mbalimbali ambapo ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Bi. Rukia Muwango na nafasi yake imechukuliwa na Bw. Hashim Abdallah Komba.

Magufuli pia ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Bw. Bakari Mohammed Bakari, na nafasi yake ameteuliwa Bw. Hassan Abbas Rungwa. Bw. Bakari ndiye aliyebanwa na Rais Magufuli hivi karibuni kuhusu ujenzi wa Soko la Nachingwea na Kituo cha Mabasi.

 

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemteua Bw. Mathias Kabunduguru kuwa mtendaji mkuu wa Mahakama ya Tanzania, akichukua nafasi ya Bw. Hussein Katanga ambaye ameteuliwa kuwa Balozi huku akimteua Bw. Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, akichukua nafasi ya Bw. Mathias Kabunduguru ambaye amekuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.


Loading...

Toa comment