
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, leo Ijumaa, Mei 24, 2019 amkwenda Afrika Kusini ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa.

Katika safari hiyo Magufuli ameongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.

Wakizungumza kabla ya kuondoka, Kikwete na Mangula wamesema Tanzania na Afrika Kusini zina uhusiano mkubwa na wa kihistoria na kwamba serikali na chama vina kila sababu ya kudumisha uhusiano na ushirikiano huo.
Viongozi hao wametumia ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Aidha, Prof. Kabudi amesema baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Ramaphosa, Rais Magufuli atafanya ziara ya kitaifa nchini Namibia ambako pia atazindua mtaa uliopewa jina la Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kutambua mchango wake kusaidia nchi za Afrika kupata uhuru.
View this post on Instagram
View this post on Instagram


Comments are closed.