The House of Favourite Newspapers

JPM Asema: Usajili Laini za Simu Kwa Vidole ‘Hilo Haliwezakani’ – Video

RAIS John Magufuli  ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano nchini (TCRA) kutowabughudhi wananchi ambao hawana vitambulisho vya taifa katika zoezi la kusajili laini za simu kwa kutumia mfumo wa utambuzi wa alama za vidole ambalo limepangwa kuanza Mei 1, mwaka huu na kwamba zoezi hilo haliwezekani kukamilika katika muda ambao awali uliwekwa na mamlaka husika.

 

Rais ametoa kauli hiyo leo Aprili 25, 2019, jijini Mbeya wakati, akizungumza na wananchi wa Mbeya na kusema kwamba zoezi hilo haliwezi kufanyika kama ilivyopangwa na TCRA kwa kuwa sio watu wote wanaomiliki simu wana vitambulisho vya taifa na akiitaka Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) kuongeza kasi ya kuwapatia wananchi vitambulisho hivyo.

 

“TCRA wamesema watu wasajili simu kwa kutumia Vitambulisho vya Taifa… Watanzania tupo milioni 55, waliopata vitambulisho ni milioni 14, unaposema lazima Watanzania wasajili laini za simu kwa kitambulisho cha taifa na wakati NIDA hawajamaliza kutoa vitambulisho kwa Watanzania,  hii haiwezekani, hii ina maana ya kuwaeleza Watanzania mamilioni wasiwe  na simu.  Lazima zoezi la kutoa vitambulisho liende na usajili,” alisisitiza na kuongeza:

 

“Wanachokifanya TCRA ni kitu kizuri ili kupunguza na ujambazi pia, lakini ninawaambia TCRA na wizara inayohusika, jambo wanalolifanya ni zuri sana lakini waanze na wale milioni 14 walio na vitambulisho vya taifa na zoezi la kusajili liende mpaka Desemba, ili liendane sawa na utoaji wa vitambulisho vya taifa.”

VIDEO: MSIKIE MAGUFULI AKIFUNGUKA

Comments are closed.