The House of Favourite Newspapers

Jukwaa la KAN Lawa Gumzo Kwa Wapenzi wa Burudani

0

Ubunifu uliotumika kutengeneza jukwaa kuu la Knowledge, Art na Networking (KAN) umekua kivutio kikubwa kwa wapenzi wa sanaa na burudani ya kupambwa na miamvuli ya rangi tofauti tofauti ikisindindikizwa na michoro inayong’ara ikionesha watu wakicheza kwenye ukuta wa jukwaa.

Akizungumza kuhusu jukwaa hilo Mkurugenzi wa tamasha hilo Dave Ojay amesema kupamba jukwaa hilo na baadhi ya maeneo mengine kwa kutumia miamvuli kunaendana na kauli mbiu ya mwaka huu Maendeleo ni watu si vitu.
Alisema, miamvuli imechukuliwa kama mfano wa mti unaoleta kivuli kwenye maisha ya watu.

Sanaa inayotumika kuchora maua yanayopambwa na rangi tofauti tofauti kwenye mwamvuli inawakilisha ‘art’ pamoja na vyuma vinavyofunguka na kufunga mwamvuli ukifunguka unawakilisha ‘network’ .

“Ubunifu wa kupamba kwa kutumia miamvuli inaendana na kauli mbiu ya tamasha ambapo sanaa ya kupata maua kwwenye miamvuli hiyo pamoja na vyuma vinavyoachana na kushikana wakati mwamvuli ukifungwa na kufunguliwa viinashiria nertworking,” alisema Ojay.


Kivuli cha miamvuli kinatasfiri maendeleo ya maisha ya mtu kama ilivyo kauli mbiu inayojadili mambo mbalimbali ya maendeleo yanahitaji pia kivuli ikiwa ni pamoja na malazi, makazi na chakula.


Msimu wa pili wa tamsha hili ulianza tatehe 22 na unafika kileleni leo ambapo wasanii wanne watahitimisha kufungwa kwa tamasha hilo. Wasanii hao ni Fid Q, ktuoka Tanzania, Isabella Novella kutoka Mozambique, Victor Kunonga kutoka Zimbabwe, Bengatronics an Tear Drops kutoka Kenya.

Leave A Reply