The House of Favourite Newspapers

Jukwaa la Katiba: Magufuli Rejesha Mchakato wa Katiba Mpya

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba nchini, Deus Kibamba akizungumza na wanahabari.

JUKWAA la Katiba Nchini limemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuurejesha Mchakato wa Katiba Mpya ili ijadiliwe na wananchi.

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba, alisema leo kuwa hiyo inatokana na mapendekezo ya mkutano wao mkuu wa kitaifa ulifanyika Machi 3 na 4 mwaka huu ambao ulihusisha wajumbe mbalimbali wakiwemo wabunge, wawakilishi wa vyama vya siasa, taasisi za elimu ya juu, mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia, dini na makundi mengine ambao jumla yao walikuwa 150.

Alisema kuwa katika mkutano huo, kuliwasilishwa na mada mbalimbali kuhusu historia ya katiba na uandishi wake Tanzania, matakwa ya maslahi Zanzibar katika mchakato, maudhui ya katiba mpya, mkwamo katika mchakato na namna bora ya kuutatua.

Alifafanua kuwa miongoni mwa maamuzi ya mkutano huo ilikuwa kushauri kuwa kwa nafasi yake, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ndiye mtu pekee kwa sasa mwenye uwezo wa kuamua hatma ya ama kuokoa au kuangamiza mchakato wa katiba mpya nchini.

“Rais alitangazie Taifa juu ya tarehe rasmi ambayo mchakato wa katiba mpya utarejeshwa ikiwemo kuagiza kuchapishwa kwa tangazo lake katika gazeti la serikali,” alisema.

“Serikali itenge fedha kuanzia bajeti ya mwaka 2017/2018 katika fungu la Wizara ya Katiba na Sheria ili kuwezesha shughuli za awali katika kurejesha mchakato wa katiba mpya kuweza kuanza,” alisema.

Kwa taarifa kamili tembelea www.globaltvtz.com.

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.