The House of Favourite Newspapers

Zanzibar Yaanza Kulipa Deni la Umeme

Rais Magufuli

DAR ES SALAAM:  SERIKALI ya Zanzibar imelipa Sh. bilioni 10 ikiwa ni mwanzo wa kulipa deni kubwa inalodaiwa na shirika la umeme nchini (Tanesco). 

Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter  Muhongo, jijini Dar es Salaam kufuatia mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, John  Magufuli na Rais wa Zanzibar, Ali Mohammed Shein yaliyofanyika Ikulu leo Dar es Salaam kuhusu deni la Zanzibar.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na  Muhongo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Kahitwa Bishaija na Meneja Mwandamizi wa Fedha wa Tanesco, Sadock Mugendi.

Pamoja na kuwatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuwa hawatakatiwa umeme baada ya kuanza kulipwa kwa deni hilo, Muhongo amewataka pia wadaiwa sugu wote wa shirika hilo kulipa madeni katika kipindi cha siku tano zilizobaki kwa kuwa wasipolipa watakatiwa umeme.

 

Comments are closed.