Julio: Simba Msiwafananishe Waarabu na Ndanda

Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

KOCHA wa Dodoma FC na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefunguka kuwa wachezaji wa Simba wanatakiwa kuwa makini na wasiwachukulie poa Waarabu kwa kuwafananisha na Ndanda, Mbao au Lipuli.

 

“Unajua Simba wapo vizuri sina hofu nao ila wanatakiwa kutovimba vichwa sana wajue wanakwenda kukutana na Mwarabu ambaye kama anajua basi ujue anajua na wanaakili wale hivyo wanatakiwa kuwa makini sana na wasijaribu kuwafananisha na Ndanda, Mbao au Lipuli na mwisho wa siku yakawa mengine.

“Wajue kuwa wanaenda kukutana na timu ambayo hawaifahamu zile clip za mitandaoni zinazosambaa waachane nazo na wala wasiwadharau wapinzani wao cha msingi wajipange na kuona ni jinsi gani wanafanya vizuri.

 

“Lakini kufanya kwao vizuri kutatokana na sapoti ambayo watapata kutoka kwa mashabiki wa klabu pamoja na Watanzania kwa ujumla ambao tunatakiwa kuungana na kuwa kitu kimoja kuifanya timu ifanye vizuri sababu inawakilisha nchi.”alisema Julio ambaye ni mwanachama wa Simba.

STORI NA MARTHA MBOMA

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment