The House of Favourite Newspapers

Jundokan Tanzania Karate-Do Yafunguliwa Mipaka Japan, Yapewa Mwaliko Sweden

0
Kutakuwa pia na semina maalum kwa wana Jundokan wote toka miji ya Dar es salaam, Dodoma na Mafinga, Iringa, Tanzania na kufanya mitihani ya ngazi mbalimbali

KWA MUJIBU wa habari toka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Karate cha Jundokan So Honbu chenye makao yake makuu mjini Naha, Okinawa, Japan master Kancho Yoshihiro Miyazato. Baada ya miaka karibuni mitatu sasa walimu wa karate toka Japan, walizuiliwa kutoka nje  na pia kuingia kwa wageni nchini Japan kutokana na janga la ugonjwa wa Corona, Covid-19 (UVIKO-19).

 

Serikari ya Japan, imeamuru kuanzia mwezi Juni, 2022 watu wataruhusiwa kutoka na pia kuitembelea nchi ya Japan, baada yakutoa vikwazo vya safari hizo kwa muda mrefu. Hii imewapa nafasi wafuasi wa Karate duniani kuanzisha safari zao kutembelea katika chimbuko la Karate duniani, visiwa vya Okinawa.

 

Hivyo, kwa mujibu wa taarifa ya chama cha Jundokan, Walimu Wakuu (Masters) Kancho Miyazato, sensei Tetsu Gima, sensei Tsuneo Kinjo, Sensei Kazuya Higa,   sensei Takayuki  Miyakozawa na  sensei Aono wa chama hicho toka mjini  Naha, Okinawa, watajumuika na Walimu wote wa Bara la Ulaya, Marekani na Afrika katika semina ya mafunzo ya kila mwaka (Gasshuku) mjini Enkoping, Sweden yatakayo fanyika  tokea tarehe 7 hadi 10 mwezi Julai, 2022 ikiwemo nchi za Tanzania, Afrika ya Kusini  na Angola.

Jundokan Tanzania Karate-Do yaruhusiwa tena kuingia katika nchi ya Japan, Semina itakuwa nchini Sweden

Kutokana na maelezo ya mkuu wa tawi la chama hicho cha Jundokan Tanzania (Shibu-Cho) Sensei Fundi Rumadha, alieleza kwamba kutakuwa pia na semina maalum kwa wana Jundokan wote toka miji ya Dar es salaam, Dodoma na Mafinga, Iringa, Tanzania na kufanya mitihani ya ngazi mbalimbali za mikanda mieusi kwa wanafunzi takribani tisa au kumi watakao panda ngazi toka mkanda mweusi hatua ya kwanza yaani “Shodan”, hatua ya pili “Nidan”, nah atua yatatu “Sandan”, digrii ya kwanza hadi ya tatu. Baada ya kuhitimu ngazi ya daraja la tatu yaani “Sandan:, majina yote na orodha yao huthibitishwa kwa mwenye kiti wa chama hicho Kancho Yoshihiro Miyazato mwenye mamlaka ya kuwafanyia mtihani wa daraja la nne hapo miaka ya baadae kupitia maandalizi maalum ya moja kwa moja toka Okinawa kwa “Zoom” chini ya usimamizi wa sensei Fundi Rumadha.

 

Wanafunzi wa tarajiwa kupandishwa ngazi watatajwa majina yao baada ya kuhitimu mitiani yao  mwezi wa Juni  mjini Dar es salaam.

 

 

 

 

 

 

 

Leave A Reply