The House of Favourite Newspapers

Jux Kuvuta Jiko Soon

0

HAYAWI hayawi yanakwenda kuwa! Megastaa wa RnB Bongo, Juma Mussa ‘Jux’ amevunja ukimya kuwa muda umefika wa kuvuta jiko.

 

Akipiga stori na OVER ZE WEEKEND, Jux amethibitisha kuwa na uwezo wa kumtunza mwanamke kwa kila kitu hivyo haoni sababu ya kumzuia yeye kuwa ndani ya ndoa.

 

“Mimi ni mwanaume imara ambaye nina uwezo kumuhudumia mwanamke maana kwangu atakula, atakunywa, atavaa na hata vitu vingine atapata. Kuoa ni baraka kubwa hapa duniani na hicho ndicho kifuatacho,” anasema Jux ambaye baada ya kutengana na Vanessa Mdee aliangukia kwenye penzi la mrembo Nayika wa Thailand kabla ya kudaiwa kuminya na sosholaiti wa Kenya, Huddah Monroe.

STORI: KHADIJA BAKARI

Leave A Reply