The House of Favourite Newspapers

Kada wa CCM abebwa juu kutimiza ahadi aliyotoa!

0

Kada mmoja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aitwaye mama Pili a.k.a Bonge, mkazi wa Keko Dar, juzi alibebwa juu na masela wanaokipenda chama hicho kisa kutimiza ahadi aliyoitoa kama Dk. John Magufuli akiingia ikulu.

Habari kutoka kwa shuhuda wa kitimbi hicho zinapasha kwamba, baada ya Magufuli kutangazwa mshindi hadi kuapishwa mama Pili aliyewaahidi masela hao kuwapa bia za kutosha hakuwepo jijini.

“Juzi mama Pili aliporejea kutoka kwao Kigoma, akiwa na furaha ya Magufuli kuingia ikulu alinunua kreti tatu za bia ambazo alikunywa na masela ambao walilewa na kumbeba juu huku wakimsifia kwa kutimiza ahadi aliyotoa,” alisema shuhuda huyo.

Leave A Reply