The House of Favourite Newspapers

Kagera Sugar, Mwadui warejea Ligi Kuu

Kagera Sugar

KAGERA na Mwadui zimerejea rasmi kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kushinda mechi zao wa mtoa jana Jumamosi dhidi ya timu za Daraja la Kwanza. Kagera iliwashinda Pamba huku Mwadui ikiwachapa Geita.

 

 

Mchezo huo wa marudio wa Kagera ulichezwa uwanja wa Kaitaba na ulikuwa na ushindani mkubwa kwani kipindi cha kwanza Pamba waliwakazia Kagera Sugar ambao msimu uliopita waliwapiga mabingwa Simba nje ndani.

 

Kikosi cha timu ya Mwadui

Mabao ya ushindi kwa Kagera Sugar yalipachikwa kiminani na Ali Ramadhani dakika ya 50 baada ya kukusanya kijiji cha mabeki wa Pamba na kuachia bonge moja ya shuti akiwa ndani ya 18 kabla ya Japhet Makalayi kupachika bao la pili dakika ya 78 na kufanya washinde kwa mabao 2-0.

 

Uwanja wa Kaitaba ulikuwa na shangwe kubwa jana huku mashabiki wakionekana kugawanyika pande mbili. Baadhi ya mashabiki waliokuwa wakiishangilia Pamba walikuwa wa Simba ambao walikuwa wanadai bora Kagera ishuke kutokana na kile walichowafanyia kuwafungia nje ndani msimu uliopita.

 

Lakini wale wa Yanga walitaka Kagera ashinde kwa madai kuwa inawafurahisha. Katika mchezo wa Mwadui, Salim Aiyee mshambuliaji aliwafungia mabao mawili yaliyoibakiza timu yake kwenye ligi katika mchezo uliochezwa uwanja wa Mwadui Complex dhidi ya Geita FC zote za Kanda ya Ziwa.

 

Mwadui FC walianza safari dakika ya 32 kupitia kwa mshambuliaji mwenye spidi ya ajabu, Aiyee kabla ya Geita kusawazisha dakika ya 50 kupitia kwa Baraka Jerome na Aiyee tena kufunga bao la usiku dakika ya 90 na kuonyeshwa kadi ya njano kwa kosa la kuvua shati. Mechi hizo mbili zilikuwa na hamasa kubwa ya mashabiki.

Comments are closed.