The House of Favourite Newspapers

Basi Laingia Dukani Kahama, Abiria Saba Wanusurika

ABIRIA saba wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamenusurika kifo baada lori la mizigo aina ya Fuso lenye namba  za usajili T 322 ACC walilokuwa wakisafiria kugongana na basi aina ya Scania lenye namba za usajili T 245 AJS liitwalo Kwela Classic, mali ya Laurent Ncheye mkazi wa Kahama linalofanya safari kati ya Kahama na Kigoma.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanya, Richard Abwao, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo asubuhi baada ya dereva wa basi hilo kuligonga lori hilo lilokuwa limebeba magunia 100 ya mahindi katika eneo hilo na kusababisha lori hilo kupinduka na kusababisha majeruhi wa ajali hiyo.

 

Amesema majeruhi hao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Halmashauri ya mji wa Kahama na hali zao zinaendelea vizuri na amewataka madereva wote wilayani humu kuheshimu alama za barabarani hususani wanapotaka kuingia katika makutano ya barabara ili kuzuia ajali.

 

Amesisitiza  kwamba chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo kutochukua tahadhari pindi alipongia katika makutano ya barabara kwa mwendo kasi na kusababisha ajali hiyo ambayo imeharibu miundo mbinu ya barabara na nyumba za watu zilizopo karibu na eneo hilo.

 

Amefafanua kuwa dereva wa basi hilo amejisalimisha katika kituo cha polisi Kahama na baada ya kuhojiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinayomkabili.

 

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama Dkt, George Masasi amesema amepokea majeruhi hao saba na hali zao zinaendelea vizuri ambao ni pamoja na dereva wa lori hilo ambao wameumia katika sehemu mbalimbali.

 

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Amos Joseph,  amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 11 alfajiri baada ya dereva wa basi kupita katika eneo hilo kwa mwendo kasi kwa lengo la kuwahi abiria katika kituo kikuu cha mabasi cha Kahama na kusababisha abiria waliokuwepo katika lori hilo kujeruhiwa huku basi likiparamia duka.

 

NA SALVATORY NTANDU

 

 

BREAKING: JAGUAR AKAMATWA NA POLISI, KAULI YAMPONZA!

Comments are closed.