The House of Favourite Newspapers

Kajala Anaishi Kama Yuko Mbele Vile!

0

MMOJA kati ya mastaa wa Bongo Muvi wanaoishi kama ‘mamtoni’ ni Kajala Masanja ambaye amefanikiwa kujijenga misingi imara ambayo imemwezesha kuishi maisha mazuri kama yuko mbele vile! RISASI linakupalia.Hayo yamethibitishwa hivi karibuni kutokana na uzuri wa nyumba anayoishi na samani zilizomo ndani ya nyumba hiyo iliyopo maeneo ya Mbezi Salasala, jijini Dar.

 

RISASI lilifanya uchunguzi wa kina katika makazi ya mlimbwende huyo baada ya kutinga nyumbani kwake na kujionea mwenyewe jinsi anavyoishi maisha ya kiwango cha juu.

 

Uthamani wa nyumba hiyo, mpangilio wa nyumba yake na vitu vya thamani kama samani za ndani, kitanda anacholalia sio chini ya milioni tatu na ushee.

Aidha, Kajala pia anasifika kwa usafi wa kipekee hususani kutokana na mpangilio mzima wa nyumba hiyo.

Uchunguzi wa RISASI umebaini kuwa msanii huyo sasa anamiliki gari aina ya Harrier New Model ilihali nyumba ya anayoshi analipa kodi zaidi ya milioni 20 kwa mwaka.Pamoja na hilo, ameitengenezea nyumba hiyo garden (bustani) ya kisasa ambayo inampa uwezo wa kujinafasi kwa upepo mwanana na hata kufanya mazoezi ya hapa na pale.

Mpashaji wetu mmoja ambaye yuko karibu na Kajala, alisema msanii huyo ana tabia ya kubadili samani zilizopo ndani ya nyumba hiyo kila mwaka na kila atakachokiweka kina thamani kubwa inayoifanya nyumba yake kuvutia wakati wote.“

 

Yaani mimi napajua majumbani wanapoishi mastaa mbalimbali wa Bongo, lakini kwa Kajala panaweza kukawa panaongoza kwa upande mastaa kwa sababu anaipenda nyumba anayoishi ndiyo maana ameigharamia kwa vitu vingi vya thamani,” alisema mpashaji huyo.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

Leave A Reply