The House of Favourite Newspapers

Kajala: Upweke wa Paula unanitesa

0

KAJALA Masanja au Frida Kajala; ni mwanamama wa Bongo Movies ambaye anasema kuwa, hakuna kitu kinachomtesa kama upweke wa kummisi mwanawe kipenzi, Paula ambaye yupo masomoni nchini Uturuki. Hii ni kwa sababu Paula ndiye alikuwa naye na ni rafiki mkubwa kwake.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Kajala anasema kuwa, anajitahidi mno kusahau na kuwa bize na mambo mengine, lakini ukweli ni kwamba anammisi mno.

 

Anasema kutokana na upweke huo, yeye anachofanya ni kumuombea ili aweze kumaliza masomo yake salama na arejee nyumbani, waungane tena kama zamani.

 

“Ni kweli naweza kusema upweke wa kutokuwepo kwa Paula unanikabili, lakini ninachofanya ni kumuombea kwa Mungu siku zote arejee salama na afaulu masomo yake vizuri kwa sababu ukweli ni kwamba nimmemisi sana na nimepata upweke mkubwa kwa sababu ndiye rafiki yangu kipenzi,” anasema Kajala ambaye hana rafiki mkubwa zaidi ya Paula.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply