Kanye Huenda Akatupwa Jela

VYOMBO mbali mbali ulimwenguni, ukiwemo mtandao mkubwa wa habari wa @tmz_tv ambao umeripoti kuwa, Idara ya Polisi jijini Los Angel wanafanya uchunguzi kuhusiana na shtuma zinazo mkabili rapa @kanyewest.

 

Hii ni baada ya kumpiga Shabiki aliyekuwa akiomba saini (autograph) ya Rapa huyo. Mashtaka hayo yamefikishwa asubuhi ya jana Alhamisi katika Idara ya Polisi jijini Los Angel.

 

Hii si mara ya kwanza Kanye kukutana na zahama kama hili, mwaka 2014 alishtakiwa kuhudhuria session 24 za Anger Management (Menejimenti ya Saikoloji Kuhusiana na Mambo ya Hasira) na kufanya kazi za kijamii kwa masaa 250 baada ya mwaka 2013 kuvunja Camera ya paparazi aliyejulikana kwa jina la Daniel Ramos.

 

Kanye West bado hajakamatwa kuhusiana na sakata hili, na endapo atakutwa na hatia, basi anaweza kwenda jela kwa miezi 6.


Toa comment