The House of Favourite Newspapers

Kanye West Anaendelea Kuwapiga Watu Hela

0

HUENDA Agosti 15, mwaka huu mashabiki wasiipate album mpya ya rapa maarufu duniani, Kanye West, #DONDA bali wajipange kwenda uwanjani tena kushuhudia uzinduzi wa album hiyo.

 

Jana Jumatatu rapa Kaycyy ambaye anafanya kazi kwa ukaribu na Kanye kwenye project hii ya DONDA, aliandika na kufuta kupitia ukurasa wake wa twitter kwamba “Tunahamia kwenye uwanja mwingine.” Inaonekana hii inamfaidisha vizuri Kanye kabla hata ya kuipeleka album yake sokoni.

 

Mickey Drexler, CEO wa zamani wa kampuni ya GAP ameuambia mtandao wa Yahoo kwamba kampuni hiyo ya mavazi iliingiza kiasi cha ($7 million) takribani TZS. Bilioni 16.2 kwa usiku mmoja kufuatia mauzo ya Majaketi (Yeezy & Gap Jacket) ambapo uzinduzi wake ulienda sambamba na uzinduzi wa album ya DONDA, August 5 mwaka huu kwenye uwanja wa Mercedes Benz.

 

Jumla ya oda 35,000 zilifanyika usiku huo kwenye tovuti ya kampuni ya GAP, huku Jaketi moja likiuzwa kwa ($200) takribani TZS. 463,800.

Leave A Reply