The House of Favourite Newspapers

Kanye West Apata Chombo Kipya

0

MBALI na kusambaa kwa taarifa za kwamba rapa maarufu duniani kutoka nchini Marekani, Kanye West anahangaika kurudisha ihusiano wake na aliyekuwa mkewe, Kim Kardashian jambo lililomfanya anunue mjengo mpya karibu kabisa na eneo analoishi mwanamama huyo ili awe naye karibu, taarifa mpya zimeibuka na kuzua maswali.

 

Kanye West ameibua mijadala miongoni mwa mashabiki wake na watumiaji wa mitandao ya kijamii mara baada ya rapa huyo kuonekana akiwa na mrembo na muigizaji maarufu nchini humo, Julia Fox.

 

Couple hiyo imeonekana kwenye mgahawa wa hadhi kubwa huko Miami nchini Marekani wakila bata huku wote wawili wakionekana ku-enjoy maisha ya kuwa pamoja.

 

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii nchini humo zinaeleza kuwa, Kanye anajaribu kujiburudisha baada ya kuachana na Kim kwa kufuata misingi ya sheria ya nchi hiyo.

 

Kanye na Kim walifunga ndoa rasmi mwaka 2014 na kuishi pamoja kama mke na mume mpaka mwaka jana 2021 walipoamua kutalakiana wakiwa wamejaliwa kupata watoto wanne, wa kike North wa kike (7), Saint wa kiume (5), Chicago wa kike (3), pamoja na Psalm wa kiume (2).

Leave A Reply