The House of Favourite Newspapers

Kapombe Aumia Tena Akiwa Mazoezini, Huenda Akaikosa AFCON

BEKI wa klabu ya Simba na Taifa Stars, Shomary Kapombe,  ameumia tena kwenye mazoezi ya timu ya Taifa ambayo yalikuwa yanafanyika Uwanja wa Taifa.

 

Kapombe alikuwa nje ya uwanja kwa majeraha ambayo aliyapata mwisho wa mwaka jana kwenye kambi ya timu ya taifa akijiandaa na mechi dhidi ya Lesotho.

Taarifa zinasema amejitonesha kwenye mazoezi maalum aliyokuwa akifanya chini ya uangalizi wa madaktari wa timu ya Simba na Taifa Stars na anaweza kukosekana kwenye msafara wa wachezaji wa Tanzania ambao Juni 7 wataelekea nchini Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya ainali za Mataifa Afrika (Afcon 2019).

Comments are closed.