The House of Favourite Newspapers

Karafuu, Strawberry kwa Meno Meupe!

KATIKA urembo leo tutaona jinsi ya kupata meno meupe kwa kutumia karafuu na strawberry kama utatumia wakati wa kupiga mswaki.

STRAWBERRIES:

Chukua kipande cha tunda hilo, kisugue kwenye meno yako yote na baada ya hapo acha kwa muda wa dakika 10 kisha sukutua au piga mswaki wako kama kawaida. Unaweza kutumia tunda hili kila siku au mara mbili kwa wiki.

LIMAO:

Limao pia ukilichukua, ukasugua meno yako husaidia kung’arisha meno. Lakini pia limao husaidia kwa kuondoa harufu mbaya mdomoni. Unachotakiwa kufanya, chukua juisi ya limao sukutua mdomoni acha kwa dakika 5 kisha piga mswaki wako, kama utakuwa umeyasugua meno kwa kipande cha limao pia acha kwa muda wa dakika tano.

MAJANI YA NANAA:

Majani ya nanaa nayo ni mazuri kwa kung’arisha meno, chukua majani hayo sugua meno yako ukimaliza chukua dawa ya mswaki na uswaki. Fanya hivyo mara kwa mara, nanaa huondoa rangi ya njano kwenye meno na kuyarudishia weupe wake.

KARAFUU:

Karafuu zichukue punje kadhaa zisage kisha unga wake weka kwenye mswaki sugua meno yako yatakuwa meupe lakini utakuwa umeyalinda na wadudu.

Comments are closed.