The House of Favourite Newspapers

KAULI YA DK MASHINJI BAADA YA MAALIM SEIF KUTIMKIA ACT WAZALENZO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Vincent Mashinji amempongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) kwa maamuzi yake ya kujiunga na Chama cha ACT- Wazalendo na kusema uamuzi wake ni sahihi.
 
“Nimpongeze kwa uamuzi wake wa kuendelea na shughuli za kisiasa na kupigania mabadiliko kwenye taifa letu, watu wengi walitegemea yeye kupumzika lakini amejipima na ameona anahitaji kuendelea kufanya kazi ni hatua kubwa kwetu sisi wapinzani,” amesema  Dkt Vincent Mashinji.
Mapema leo Machi 18, 2019 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, ilitangaza kutambua uhalali wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba.
Kufuatia maamuzi hayo ya Mahakama,  majira ya saa nane leo Machi 18, 2019  Maalim Seif alitangaza uamuzi wa kuhamia Chama Cha ACT – Wazalendo.

Comments are closed.