The House of Favourite Newspapers

Kazi Imeanza!

0

MAGUFURI (11)Rais Jakaya Kikwete (kushoto) na rais mteule wa awamu ya tano, Dk John Pombe Magufuli (kulia).

ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS

JANA, aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli (56) alikabidhiwa cheti cha kuutambua ushindi wake wa nafasi hiyo baada ya kuibuka na kura nyingi kwenye uchaguzi uliyofanyika Oktoba 25, mwaka huu huku watu wakisema kitendo cha kumkabidhi cheti kazi imeanza.

MAGUFURI (7)Rais mteule wa awamu ya tano, Dk John Pombe Magufuli akionesha cheti cha ushindi wa urais kwa aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo, Mghwira.

Hafl a ya kumkabidhi cheti Magufuli ilifanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar kuanzia saa nne asubuhi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, waangalizi wa kimataifa (akiwemo rais mstaafu wa Nigeria, Gudlucky Jonathan), pia wakiwemo waliokuwa wagombea wengine wa nafasi ya urais. Viongozi waliohudhuria ni rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete ‘JK’, Spika wa Bunge, Anna Makinda, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Jaji Joseph Warioba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik na makamu mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula.

Shughuli hiyo ya kukabidhi cheti ilifanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (Nec) chini ya mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu Damian Lubuva. Baadhi ya wanachama wa CCM ukumbini humo walisikika wakisema kuwa, wezi wa mali za umma, wategaji wa kazi na wazembe, wajiandae, Magufuli ameshapewa, kazi imeanza rasmi.

MAGUFURI (4)

Rais mteule wa awamu ya tano, Dk John Pombe Magufuli na Makamu wake, Bi Samia Suluhu wakipongezana mara daada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi.

Hata hivyo, baada ya rais JK kukaa, baadaye msafara wa waliokuwa wagombea wa urais uliingia ambapo ni Anna Mghwira wa ACT-Wazalendo, Fahmi Dovutwa wa UPDP, Janken Kasambala wa NRA, Lutasolwa Liyemba wa ADC na Magufuli wa CCM. Edward Lowassa aliyekuwa mgombea wa Chadema akiungwa mkono na Ukawa, Hashim Rungwe aliyegombea kupitia Chaumma na Maxmillian Lyimo aliyegombea kwa chama cha TLP hawakuhudhuria. Baada ya wagombea hao kukaa, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani alizungumza halafu akamkaribisha Jaji Lubuva ambaye alieleza kwa kifupi mchakato mzima wa uchaguzi ulivyokuwa tangu kupiga kura hadi kutangaza mshindi juzi.

Baadaye alitoka eneo la kutangazia na kwenda kumkabidhi cheti Dk. Magufuli ambaye naye alipita ukumbini kuwaonesha watu mbalimbali akianzia na wagombea wenzake mpaka kwa mkewe, Janet Magufuli aliyekaa jirani na mke wa JK, mama Salma.

Pia, mama Anna Mghwira alipewa nafasi ya kusema neno kwa niaba ya wagombea wengine ambapo alisema amekubali matokeo na kumtaka Magufuli kufanya mabadiliko ya kweli na kusimamia umoja wa kitaifa na alisema anataka katiba mpya huku akimpa Ilani ya Uchaguzi ya ACT kwa ajili ya kuchukua mambo muhimu na kuyafanyia kazi.

Baada ya zoezi hilo, shughuli ilimalizika kwa Magufuli kupiga picha na viongozi mbalimbali, wadau na waangalizi wa kimataifa pia na wagombea wenzake na kuondoka kuelekea Ofi si Ndogo za Chama Cha Mapinduzi zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar.

Huko, viongozi wa juu wa chama hicho, akiwemo mwenyekiti JK na wanachama waliovalia sare walikuwa wakimsubiri. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipanda jukwaani baada ya Magufuli kufi ka na kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulhaman Kinana ambaye alitoa neon kidogo na kumkaribisha JK.

Kwa upande wake, JK alidhihirisha furaha yake kwa kusema amefurahi sana kwa sababu kuna watu walishasema chama kitamfi a mkononi.

“Nimefurahi sanasana. Maana kuna watu walisema CCM itafi a mikononi mwangu. Siri ya ushindi wetu ni kubwa. Hakuna mwana CCM aliyekuwa anatumia viroba.

“Kazi ilikuwa ngumu, lakini imekwisha salama. Wengine waliamua kuhama chama kwenda kutafuta riziki kwingine nako mambo hayakwenda vizuri,” alisema JK huku akishangiliwa. Baada ya JK, Mafuguli alipanda jukwaani na kutoa neno ambapo aliwashukuru Watanzania wote kwa ujumla, wana CCM na wa vyama vingine akisema kilichobaki sasa ni kazi tu!

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya wanchama wa CCM wakati wote wa hotuba ya Magufuli walikuwa wakizungumzia waziri mkuu atakayeweza kufanya kazi na kiongozi huyo. Walikuwa wakiwataja mawaziri mbalimbali wanaoweza kufanya kazi na Magufuli huku mawaziri watatu (JM, HM na WL) wakitajwa zaidi.

Leave A Reply