The House of Favourite Newspapers

Nyumba Ya Diamond si yake

0

DIAMOND TIFFAH'S 40 (5)

Nyumba ya Diamond inayodaiwa si yake.

GLADNESS MALLYA IMELDA MTEMA

IMEVUJA! Ile nyumba ya kifahari iliyoaminika ni ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ imefahamika kuwa siyo yake kama wengi walivyokuwa wakifahamu.

diamond (2)Diamond Platinumz.

Kuvuja kwa siri hiyo kumetokana na maneno ya wambeya yaliyokuwa yakielekezwa kwa mama mzazi wa staa huyo, Sanura Kasimu ‘Sandra’ mitandaoni kwamba kwa nini asiondoke kwenye nyumba hiyo na kumuacha mwanaye awe huru ndipo mwanahabari wetu alipomtafuta mama Diamond na kumuuliza kuhusu maoni ya wambeya hao, bi. mkubwa huyo akasema hawezi kuondoka kwani nyumba hiyo siyo ya Diamond bali ni mali yake.

nyumba ya diamondNyumba ya Diamond inayodaiwa si yake.

“Kwa taarifa yenu hii nyumba ni ya kwangu na makaratasi yote yameandikwa jina langu hao wanaosema nimwache Nasibu awe huru hawajui lolote, mimi ndiyo nimesimamia kila kitu na Nasibu hakuwahi kusimamia hata siku moja, hii ni nyumba yangu.

“Wanaosema awafukuze ndugu zake nawaambia kwamba hapa hakuna mtu atakayetoka, mwanangu nimeteseka naye hakuna anayejua tumetokea kwenye maisha gani kwa hiyo naomba watu waache kuchonga sana,” alisema mama Diamond.

Leave A Reply