The House of Favourite Newspapers

KENYA KURUSHA SATELAITI YAKE YA KWANZA IJUMAA HII

 KENYA inategemea kurusha satelaiti yake ya kwanza Ijumaa wiki hii kutokea nchini Japan. Satelaiti hiyo inayofahamika kama First Kenyan University Nano Satellite—Precursor Flight (1KUNS-PF), ni bidhaa ya Chuo Kikuu cha Nairobi kwa kusaidiana na Chuo Kikuu cha Sapienza cha Italia na wataalam wa Shirika la Japan Aerospace Exploration Agency (JAXA) kupitia mpango unaojulikana kama Japanese Experiment Module “Kibo Programe” na taasisi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia masuala la anga za mbali (United Nations Office for Outer Space Affairs — UNOOSA). 

 

Waziri wa Elimu wa Kenya, Amina Mohamed, ataongoza ujumbe utakaoshuhudia tukio hilo. Satelaiti hiyo ya mraba yenye ukubwa wa 10-kwa-10-kwa-10, itakuwa na faida kadhaa kwa Kenya ukiwemo utabiri wa hali ya hewa, uchoraji wa ramani, uchunguzi wa mazingira na wanyama.

 

 

Pia itatumika katika kuisaidia sekta ya vyombo vya habari nchini humo. Faida nyingine ni kusaidia usimamizi na uchunguzi wa mazingira ya anga za juu na majanga mbalimbali. Profesa/Mhandisi wa Chuo Kikuu cha Nairobi, amesema satelaiti hiyo ina uzito wa kilo 1.2 na na itakuwa juu umbali wa kilomita 4,000 kutoka duniani.

 

“Satelaiti za Nano hivi sasa ni vyombo vipya vinavyotumika katika utafiti wa anga za juu na shughuli za kibiashara. Ni teknolojia mpya itakayofanyiza jukumu kubwa la uchunguzi wa baadaye kwa kutumia satelaiti,” anasema Prof. Mbuthia. Chombo hicho kimetengenezwa kwa gharama ipatayo Ksh. Milioni 100 (sawa na Tsh. 22.78 bilioni) na kitadumu kwa kati ya miezi 12 hadi 18.

Comments are closed.