The House of Favourite Newspapers

Kerr amkataa Mniger wa Yanga SC

0

KERR

Kocha Mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr.

Wilbert Molandi na Hans Mloli
KOCHA Mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, ameingilia kati usajili wa straika mpya wa Yanga, raia wa Niger, Issofou Boubacar aliyesajiliwa juzi Jumatatu.Kerr amesema haoni haja yoyote ya Yanga kufanya usajili wa mshambuliaji huyo, wakati bado wana washambuliaji wengi wazuri.

Kauli hiyo, ameitoa kocha huyo jana Jumanne ikiwa ni saa chache kabla ya usajili wa dirisha dogo kufungwa.

Mniger huyo, ameingia makubaliano ya mwaka mmoja na Yanga inayojiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kerr alisema kuwa, kutokana na idadi ya washambuliaji wanne wenye uwezo mkubwa wa kufunga na wazoefu waliopo kwenye timu hiyo, haoni haja hata kidogo ya kumsajili.

“Nimeshangazwa na Yanga kumsajili huyo Mniger anayecheza straika wakati tayari wapo kina Ngoma (Donald), Tambwe (Amissi) na wengine wawili wazuri tu.

“Usajili huo ungekuwa na umuhimu zaidi kama Yanga wangemuacha mshambuliaji mmoja wapo kati ya hao wanne, kwa maana hiyo timu hiyo inakuwa na washambuliaji watano, sasa hao wote wa nini kwenye timu?” alihoji Kerr na kuongeza:

“Huyo mshambuliaji ni mpya na simfahamu kabisa, hivyo nimepanga kumfuatilia kwa njia ya mitandao ikiwemo YouTube na Wikipedia ili kujua uwezo wake, timu alizowahi kuzichezea na idadi ya mabao aliyofunga, pia nitawasiliana na mawakala wangu mbalimbali wa nchi alizochezea ili wanieleze zaidi kuhusu kiwango chake.”

Leave A Reply