The House of Favourite Newspapers

Kesi Ndogo ya Mbowe… Jamhuri Yafunga Ushahidi Wake

0

Kutoka katika chumba cha Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, shahidi wa nne kati ya mashahidi saba wa upande wa katika kesi ndogo ndani ya kesi ya Msingi namba 16/2021 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu alitakiwa kutoa ushahidi wake mbele ya mahakama lakini upande wa Serikali ukiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Robert Kidando ameiomba mahakama kufunga ushahidi huo kutokana na kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu waliotangulia.

 

Ushahidi huo umefungwa leo Ijumaa Septemba 24, 2021 Mahakamani hapo ambapo shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ndogo ambaye ni mshtakiwa wa pili Adamu Hassan Kasekwa ameanza kujitetea.

 

Katika kesi hiyo ndogo ndani ya kesi kubwa inahusu uhalali wa maelezo yake yalivyochukuliwa na polisi baada ya kukamatwa.

 

Mawakili wa upande wa utetezi wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala waliyapinga yasipokelewe Mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka kwa madai kwamba kabla na wakati wa kuyatoa maelezo hayo mshtakiwa huyo aliteswa na kwamba maelezo hayo yalichukuliwa nje ya muda unaoruhusiwa kisheria.

Leave A Reply