KESI inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji anayotuhumiwa kutumia madawa ya kulevya imeshindwa kusikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusogezwa mbele hadi Septemba 25.
Kesi hiyo ilishindwa kusikilizwa kutokana na Manji kuchelewa kufika mahakamani. Lakini Manji alimueleza hakimu kuwa aliambiwa hakimu huyo yupo katika kikao.
Kutokana na hali hiyo, imesogezwa mbele hadi Septemba 25, ambapo Manji atapeleka mashahidi wake.
Cannavaro Amfuata Manji Mahakama ya Kisutu