The House of Favourite Newspapers

Kesi Ya Mbowe, Wenzake Watatu Utetezi Waomba Kupelekwa ‘HighCort’

0

 

Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala akizungumza na wanahabari baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo.

UPANDE wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na wenzake watatu wamewasilisha taarifa ya kusudio la kuiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ipeleke mahakama Kuu matamshi yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kama suala la kikatiba.
Wakali wa utetezi, Peter Kibatala amedai kuwa wamefikia hatua ya kuleta maombi hayo kwa sababu matamshi hayo kwa maoni yao ni kuwa yanaingilia moja kwa moja uhuru wa mahakama, ambapo siyo mahakama ya Kisutu tu bali hata mahakama itakayoenda kusikiliza shauri hilo la ugaidi linalomkabili Mbowe na wenzake.
Amedai, kwa Taasisi hiyo ni yenye nguvu na inaushawishi basi matamshi yake kwa namna yalivyotamkwa yamewafanya wateja wao waone kama wameishahukumiwa na kwamba hakuna namna yoyote wanaweza wakapata haki yao.
“Tumeomba suala hilo la iwapo au la matamshi ya Taasisi hiyo yameingilia uhuru wa mahakama na iwapo au la matamshi hayo yamesababisha kesi isiwe na mantiki tena kiasi kwamba hakuna namna ya kufanya isipokuwa kuifuta, hivyo tumeiomba mahakama hii kwa kuwa haina uwezo wa kusililiza suala la kikatiba na haina uwezo wa kuitolea uamuzi kikatiba basi tunaomba mahakama hii itusikilize na ikiridhika basi itupeleke kwenye mahakama yenye mamlaka ambayo ni Mahakama kuu. amedai Kibatala.
Wakijibu hoja hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hillar umekiri kupokea kusudio hilo na wameiomba mahakama iwapatie muda kwa ajili ya kuwasilisha majibu yao.
“Mheshimiwa Hakimu, kweli tumepokea kusudio hilo kwa njia ya maandishi, tunaomba muda na sisi tutajibu kwa njia ya maandishi.” Amesema Hillar
Hata hivyo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 27, kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa kusudio hilo na pia ameamuru siku hiyo washtakiwa waletwa mahakamaninm kutokana na mtandao kusumbua sumbua mara kwa mara.
Leave A Reply