The House of Favourite Newspapers

Khadija Kopa: Sikuachwa, Nimeachia Mimi

0

MALKIA wa muziki wa Taarab Afrika, mzaliwa wa visiwa vya mashi ya karafuu, Zanzibar, Khadija Omary Kopa almaarufu Bi Khadija amekiri kuwa hadi sasa amewahi kuwa kwenye ndoa nne tofauti.

Bi Khadija ambaye ni mama ya staa wa Bongo Fleva, Zuhura Othman almaarufu Zuchu anasema kwamba, amekuwa akiwatema wanaume wake baada ya kuhisi haridhishwi nao.

 

“Kwa talaka zangu nne, sikuachwa, nimeachia mimi. Ningewaambia, wewe mwanaume huridhishi kaa ngozi ya futi, hebu nenda. Siyo eti sikuishi nao vizuri, nimeishi na waume zangu vizuri na bahati mbaya wanaondoka na wanapojutia na kutaka kurudi, mimi sina muda nao tena,” anasema Bi Khadija.

 

Bi Khadija anasema kuwa, kuna kipindi aliomba talaka yake ya kwanza baada ya mume wake kumuacha akiwa mjamzito na kupotea kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

“Nilikwenda Mahakama ya Kadhi kuelezea, wakasema mwanaume akifikisha miaka miwili naweza nikapewa talaka, nikapewa. Nilitaka mimi mwenyewe. Kwa bahati mbaya nilipopewa talaka naye akarudi,” anasema Bi Khadija.

 

Anasema kuwa, wakati mume wake wa kwanza anarudi tayari alikuwa ameposwa na mume wa pili.

Mama Zuchu anasema kuwa, mume wake wa pili alikuwa mwenye vurugu na alikuwa na mazoea ya kulala nje mara kwa mara.

Anadai kwamba aliamua kujiondoa kwenye ndoa hiyo kwa kuhofia maisha yake huku akisema kuwa wakati mumewe aliwahi kumburuza chini akiwa mjamzito.

 

Bi Khadija anasema kuwa, baada ya kuondoka kwenye ndoa ya pili aliolewa na mwanaume tapeli ambaye hakuwapenda watoto wake.

Anasema watoto wake wakiongozwa na marehemu Omari Kopa walimshinikiza aachane na ndoa hiyo baada ya mumewe kukamatiana visu na kifungua mimba wake huyo.

 

Mkongwe huyo wa muziki yapata miaka 30 sasa, anasema kuwa, wakati anaomba mumewe huyo wa tatu talaka, aliiandika haraka ila akaanza kujuta siku tatu baadaye.

Bi Khadija anasema kwamba mume wake wa mwisho, Jaffari Ally ambaye alifariki dunia takriban miaka tisa iliyopita ndiye aliyekuwa mzuri kati ya wote.

 

Anasema marehemu Ally aliwapenda watoto wake na vilevile wanawe walimpenda pia.

Bi Khadija amewahi kuolewa na mume mwenye wake watatu tayari na kueleza kwamba hakuwahi kuzozana na wake wenzake.

 

Kwa sasa hana hamu ya ndoa kwa kuwa anahofia kukutana na mwanaume ambaye hataridhia kuwa naye. Hata hivyo, anasema wapo wanaume wengi ambao wamekuwa wakimmezea mate wakitamani kumuoa.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply