The House of Favourite Newspapers

kicheko, kilio ni sehemu ya mapenzi-2

0

happy-coupleMpenzi msomaji ni Jumatatu nyingine tunakutana kwenye safu yetu hii ya maisha na uhusiano ya XXLove.Wiki hii ni muendelezo wa mada inayojieleza hapo juu. Wiki iliyopita nilikueleza namna ambavyo unaweza kujiepusha na kuongeza tatizo kwa mwenza wako.

KWA MWANAUME
Unaweza ukafanya sehemu ya majukumu ambayo amekuwa akiyafanya mwenza wako ili kuepusha kukwaruzana naye zaidi.

Kama ni maji ya kuoga kujiwekea siku moja siyo mbaya, kama ni kutoa vyombo baada ya kula siyo tatizo. Kama ni tendo la ndoa kunyimwa siku hiyo basi vumilia, ingawa eneo hili ndipo wapenzi huzalisha tatizo kubwa na kutoka nje ya ndoa.

Yapo mambo mengi sana ambayo yanaweza yakasababisha kukwazwa, kuchukizwa na kusababisha majonzi na hata kilio ila tunapaswa tufahamu kuwa ni sehemu ya maisha yetu, ila chanzo kikubwa ni mapenzi.

Kama umekwazana na mwenza wako kiasi cha kujiona mpweke na hatimaye kuwa na simanzi, hakuna sababu ya kumchukia mwenza wako, amini siku hiyo ni mbaya kwako na kikubwa ni kujifunza kukabiliana na hali hiyo huku ukifahamu kuwa siku ya furaha au kicheko inakuja.

KWA MWANAMKE
Kama unamuona mwenza wako hayuko kwenye mudi nzuri, jaribu kujiongeza na kufanya vitu vingine kimyakimya bila kusababisha vikwazo zaidi, pika chakula mapema, kama ni nyumbani, rudi mapema na mengine fanya kwa uangalifu ili tatizo la mwanzo lisizalishe matatizo mengine makubwa.

Kwa siku kama hiyo, elewa kuwa ni sehemu ya majonzi au simanzi kwa mwenza wako. Mvumilie kwa siku hiyo moja au zaidi huku ukifahamu kuwa siku ya kicheko inakuja.

KICHEKO
Baada ya kilio ambacho umekutana nacho jana, wiki iliyopita au mwezi mmoja nyuma, basi elewa kwamba siku ya furaha nayo inakuja katika maisha yako.

Kama ilivyo kwa siku ya kilio, vivyo hivyo siku ya kicheko au furaha ikifika utajua tu kwa kuona sura ya mwenza wako, kwani siku njema huonekana asubuhi, kama mwenzako anaonekana kuwa na furaha siku hiyo, jaribu kuwa naye karibu, kuzungumza na kubadilishana mawazo ya hapa na pale kuhusu furaha hiyo, naamini hiyo ndiyo siku ya kufurahia au kurudisha upya penzi lenu kwa sababu kama ni mtoko, mtatoka wote, kama ni faragha basi mtaifurahia kwa sababu kila mtu yuko kwenye hali nzuri.
Tujifunze kuzitambua na kuzifahamu nyakati hizi mbili katika maisha ya kawaida na maisha ya uhusiano wa kirafiki na kimapenzi.

Watu wengi wanashindwa kuelewa na kuukubali ukweli huu.
Kama umekwazana na mwenza wako, jaribu kuvumilia na siyo kumsema kwa maneno mabaya na yasiyofaa.

Tukutane wiki ijayo kwenye mada nyingine nzuri na tamu, pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram kujua mengi kuhusu mapenzi.

Leave A Reply