The House of Favourite Newspapers

Kidoa Amnanga Gigy Kupukutika Msambwanda

0
Msanii wa filamu Bongo ambaye pia ni video queen, Asha Salum `Kidoa’.

Dar es Salaam: Msanii wa filamu Bongo ambaye pia ni video queen, Asha Salum `Kidoa’ amemnanga staa mwenzake, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kufuatia kupukutika kwa msambwanda wake huku yeye akiwa bado analipa.

Kidoa ameifungukia 3 Tamu kuwa Gigy aliwahi kumtambia mno kwa msambwanda wake na kujiona ni bora zaidi yake, ila hivi sasa hana jeuri kwa sababu amepigwa pasi.

Gift Stanford ‘Gigy Money’.

“Nikimtazama Gigy ninabaki kumsikitikia tu maana katika vitu vigumu kuvirudisha kwenye mwili vikitoweka ni shepu. Alikuwa na mbwembwe sana na lile kalio lake, lakini kwa sasa kwisha habari yake, mwenziye ndiyo bado nakimbiza dude,” alisema Kidoa.

STORI; MAYASA MARIWATA |AMANI

Leave A Reply