The House of Favourite Newspapers

Kiduku Apiga Chini Mapambano Mawili

0

BONDIA wa ngumi za kulipwa kutoka Tanzania, Twaha Rubaha ‘Twaha Kiduku’ amefunguka kuwa tangu
kuanza kwa mwaka huu
amelazimika kukataa ofa za kupambana mapambano mawili, kutokana na kushindwana kwenye masuala ya maslahi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kiduku alisema: “Kuhusiana na mipango ya mapambano kwa mwaka huu kwa upande wangu kila kitu kinaenda vizuri, kuna baadhi ya ofa ambazo tumezipokea na tunaendelea na mazungumzo, lakini ofa mbili kati ya hizo nimezipiga chini kutokana na kushindwana kwenye maslahi.

 

“Kwa yale ambayo bado tupo kwenye mazungumzo basi kila kitu kikikamilika tutawaweka wazi.”

Leave A Reply