The House of Favourite Newspapers

Kigogo TAKUKURU Ashindwa Kuelewana na DPP

0

WAKILI wa utetezi Elia Mwingira katika kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili Kuruthumu Mansoor ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kukamilisha upelelezi wa shauri hilo kwani mazungumzo kati ya upande wa serikali na mshtakiwa yalishakufa.

 

Hatua hiyo imekuja wakati kesi hiyo ilipokuja kutajwa mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi, Godfrey Isaya ambapo Wakili wa Jamuhuri wankyo Simon amedai kuwa, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

 

Wankyo ameeleza kuwa, upande wa utetezi uliitaarifu mahakama kuwa wameandika barua lakini hajaleta majibu mahakamani hapo ya nini kinaendelea.

 

Baada ya hoja hiyo, wakili Mwingira amedai kuwa tangu kesi hiyo ilipoanza imekua ikitajwa tu lakini wanachotaka kusikia ni kama uchunguzi umekamilika na upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi haraka kwani maongezi yalishashindikana.

 

Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Godfrey Isaya ameutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi mapema. shauri hilo limehairishwa hadi januari 20 mwaka huu ambapo litakuja kwa ajili ya kutajwa.

Leave A Reply