The House of Favourite Newspapers

Kijana Miaka 19 Abaka Mtoto wa Miaka 3, Apigwa Maisha Jela

0

AMEENDA na maji! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya kumhukumu kifungo cha maisha jela, Erasto Jailos (19) mkazi wa DDC Mbalizi wilayani Mbeya, baada ya kukiri kutenda kosa la kumnajisi mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.

 

Hukumu hiyo imetolewa mapema wiki jana na Hakimu mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Paulo Ntumo baada ya mshtakiwa huyo aliyefikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, kukiri kosa la kumnajisi mtoto huyo.

 

Mshtakiwa huyo aliyefikishwa mahakamani hapo na maafisa wa jeshi la polisi, alisomewa mashtaka yake na Mwendesha mashtaka wa Serikali, Bernadeta Thomas.

 

Akifafanua kosa linalomkabili mshtakiwa huyo, Bernadeta alisema Oktoba 22 mwaka huu katika eneo jirani na nyumbani aliyokuwa akiishi, Erasto alimbaka mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitatu.

“Kosa hilo ni kinyume na kifungu namba 130 (1), (2) e na 131 (3) cha sheria ya kanuni ya adhabu,” alisema.

 

Aidha, akisoma maelezo ya awali katika shauri hilo namba 281/2019 mwendesha mashtaka huyo alisema siku ya tukio wakati mshtakiwa akiwa amelala, mtoto huyo aliyekuwa jirani na chumba cha mshtakiwa aliingia chumbani humo ndipo mshtakiwa alipoamua kufunga mlango wa chumba chake ili kutekeleza azma hiyo.

 

“Mshtakiwa alifunga mlango kisha kumvua nguo ya ndani mtoto huyo na kumpaka mafuta ya mgando aina ya Vaseline katika sehemu zake za siri ndipo alitekeleza kitendo chake cha kumnajisi mtoto huyo.

 

“Kijana huyo alimbana mdomo mtoto huyo baada ya kuanza kupiga kelele ambapo baada ya kutimiza haja yake na kumwachia, mtoto huyo alionekana kuwa na maumivu jambo lililotiliwa shaka na mama yake baada ya kushindwa kutembea vizuri.

 

“Mama yake alimtishia kwa fimbo mtoto huyo ndipo alipoeleza kuwa ameingiliwa na mtu huyo na baada ya kuchunguzwa alikutwa na michubuko sehemu za siri hali iliyomlazimu kwenda kwenye vyombo vya kisheria,” alisema.

Baada ya kusomewa shauri hilo mshtakiwa Erasto alikiri kutenda kosa hilo sawasawa na madai ya Jamhuri kama ambavyo pia alikiri baada ya kuhojiwa na polisi alipokamatwa.

 

Aidha, baada ya mshtakiwa Erasto kukiri kosa linalomkabili mahakamani hapo, hakimu wa mahakama hiyo alimhukumu kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwake na jamii kwa ujumla.

STORI: MWANDISHI WETU

Leave A Reply