The House of Favourite Newspapers

Kila La Heri Serengeti Boys Dhidi Ya Congo Leo

serengeti-boys-kikosi

Kikosi cha Serengeti Boys.

TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo itashuka dimbani, Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Debat mjini Brazaville, kumenyana na wenyeji Kongo – Brazzaville katika mchezo wa marudiano hatua ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya fainali za U-17 mwakani Madagascar. 

Serengeti Boys iliyowasili mjini Brazaville Alhamisi ikitokea Kigali, Rwanda ilipoweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo huo wa marudiano, itahitaji hata sare ili kufuzu fainali za U-17 Madagascar baada ya awali kushinda 3-2 nyumbani Dar es Salaam Jumapili wiki iliyopita.

Tanzania haijawahi kufuzu fainali zozote za vijana Afrika ingawa mwaka 2005 Serengeti Boys ilifuzu fainali zilizofanyika nchini Gambia, kwa kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabawe, lakini ikaenguliwa kwa kashfa ya kumtumia mchezaji aliyezidi umri, Nurdin Bakari aliyekuwa anachezea Simba SC wakati huo.

Lakini utaratibu mzuri uliotumika kuunda timu ya sasa kwa kufuatilia tarehe halisi ya kuzaliwa kwa mchezaji, inaaminika unaweza kuiepusha Serengeti na majanga kama ya 2005. Kila la heri Serengeti Boys.

Mungu ibariki Tanzania.   

Comments are closed.