The House of Favourite Newspapers

Kilichonitokea Baada ya Kubakwa na Kaka Yangu-25

0

Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale Evance alipokuwa chumbani na Dorcas alipombana msichana huyo mdogo kisha kumziba mdomo kwa taulo na kufanikiwa kuipandisha juu sketi yake na kuichana nguo yake ya ndani. Je, kilifuatia nini? Endelea na mkasa huu unaoumiza…

Nikiwa nahaha kujinasua alinibana kwa nguvu na bila kutegemea akanibaka jambo lililonipa maumivu makali sana ambayo nashindwa kuyaelezea, alipomaliza haja zake aliniachia na kunipa onyo kwamba ole wangu nimwambie mtu kuhusu alichonifanyia angeniua.

Wakati nalia, alitoa shuka lililokuwa limelowa damu, akatandika lingine huku akiendelea kunisisitiza eti nikithubutu kumwambia mama au mtu yeyote, ningefikwa na mauti.

Licha ya kaka Evance kunifanyia kitendo cha kinyama ghafla alibadilika na kuwa mpole, akaanza kuniomba msamaha eti shetani alimpitia akajikuta akinifanyia vile.

Alinisihi nisimwambie mtu kwani mama yake akisikia itakuwa balaa na atagoma kumlipia ada ya chuoni, kisha akarudia kwamba pamoja na kuniomba msamaha siku nitakayotoa siri hiyo ataniua na kutoroka pale nyumbani.

Kutokana na kitisho hicho, nilitoka mle chumbani nikiwa nina maumivu makali nikaenda chumbani kwangu nikaanza kulia lakini baadaye nilihisi kama mama angenikuta ninalia kwa vyovyote vile angeniuliza sababu ambapo nisingemficha kitu na matokeo yake Evance angeniua kama alivyoahidi.

Niliamua kunyamaza na kujipa huduma ya kwanza, hata hivyo sikuweza kufanya jambo lolote kwa maumivu niliyokuwanayo. Mama aliporejea na aliponiuliza sababu za kuwa mnyonge nilimwambia kichwa kilikuwa kinauma.

Mama alinipa panadol, nilipomeza nikalala, usiku alipokuja kunijulia hali nilimwambia nilijisikia nafuu na chakula kilipokuwa tayari nilikwenda mezani kwa kujikongoja kwani bado nilikuwa nina maumivu.

Kwa kuwa sikujisikia vizuri, nilipomaliza kula nilikwenda chumbani kwangu na kuanza kutafakari kitendo cha kikatili ambacho Evance alinifanyia.

Nilijikuta najisemea moyoni kwamba kama mama angekuwa hai au baba angelikuwepo wala nisingefanyiwa ukatili ule, nikaanza kutiririkwa na machozi. Hata hivyo, kuhofia mama angeingia na kunikuta nalia nilinyamaza ambapo sikukaa muda mrefu nilipitiwa na usingizi hadi nilipozinduka kwenye saa saba.

Baada ya kuzinduka, nikaanza tena kufikiria mambo mengi niliyopitia tangu nikiwa mdogo mpaka tukio la kubakwa alilonifanyia kaka Evance niliyemuamini na kumchukulia kama kaka yangu wa damu.

Kutokana na mawazo hayo, sikuweza kupata usingizi kwa muda mrefu, nakumbuka nililala kwenye saa tisa kasoro nikashtuka kufuatia mama aliyeingia chumbani kwangu kuniita ili kujua hali yangu.

Ingawa nilihisi maumivu, nilimweleza niliendelea vizuri kisha alitoka na kwenda chumbani kwake nami nikabaki najigeuzageuza kitandani hadi saa kumi na mbili na nusu alfajiri.

Kwa kuwa bado nilihisi maumivu ya jeraha nililopata baada ya kubakwa, nilikwenda jikoni nilikochemsha maji ambayo nilijikanda kwa lengo kupunguza maumivu.

Ingawa muda huo kaka Evance alikuwa hakosekani nyumbani, nilipoamka sikumuona na sikufahamu alikwenda wapi hadi ilipofisa saa tano ndipo alirejea.

Aporejea alinikuta nimeketi sebuleni peke yangu, nilipomuona nilipatwa na hasira na kutamani kumvamia ili nimng’ate meno na kunyofoa ngozi au kiungo chochote cha mwilini mwake ili kila akiliona jeraha aukumbuke unyama alionifanyia.

Hata hivyo, nilijizuia kwa kuhofia angenifanyia kitendo kibaya kama alivyoniambia nikajikuta natiririkwa na machozi na kwenda chumbani kwangu. Kufuatia hasira nilizokuwanazo, Evance aligundua sikuwa sawa ingawa hakuwa akiingia mara kwa mara chumbani kwangu aliingia na kuniomba msamaha kwa kitendo alichonifanyia.

Aliniambia kwamba tangu aliponibaka alikosa amani ndiyo maana asubuhi aliondoka pale nyumbani kwani moyo ulimsuta sana, hivyo nimsamehe.

Nikiwa nina hasira nilimwambia kwa tukio alilofanya hakupitiwa na shetani isipokuwa alidhamiria kwa muda mrefu, akanipinga kwamba hakudhamiria.

Hata hivyo, kwa hasira nilimwambia sitamsamehe na kumweleza nitamfahamisha mama juu ya kitendo hicho.

Nilipomweleza hivyo, alinipiga mkwara kwamba siku nitakayothubutu kutoa siri hiyo ndiyo ungekuwa mwisho wangu na yeye angetoroka pale nyumbani kama alivyoniambia.

Nikiwa binadamu niliyependa kuendelea kuishi, kauli yake ilininyong’onyesha nikaamua kukaa kimya na maumivu yangu kwani nilijua hata kama ningemwambia mama asingekubali kuwa upande wangu zaidi angemtetea mwanaye.

Baada ya Evance kunitisha, alitoka mle chumbani hata nilipotoka nje sikumuona hadi aliporejea jioni na  hatukuchangamkiana kama ilivyokuwa kawaida yetu.

Wakati huo wa jioni, kidogo nilipata nafuu kwani nilijumuika na wanafamilia kufanya kazi ndogondogo hadi usiku tulikula na kwenda kulala.

Siku iliyofuata, maumivu hayakuwa makali sana tukaendelea na maisha kama kawaida lakini siku kama kumi hivi mama akiwa kasafiri nilianza kuhisi kuchoka na kupenda kulala muda mwingi.

Hali hiyo ilikwenda sambamba na kukerwa na harufu ya baadhi ya vyakula hasa samaki, maharage na nilipenda sana kunywa soda tabia ambayo sikuwa nayo.

Kadiri siku zilivyokwenda nikawa najisikia ovyoovyo na hata tarehe ambazo nilikuwa napata hedhi zilipofika zilikoma, kwa kuwa sikuwa na ufahamu wa masuala ya uzazi sikuelewa kama nilikuwa nina mimba.

Wakati huo pale nyumbani hakuwepo mtu mkubwa zaidi ya kaka Evance, Emmy, mimi na msichana mwingine mtoto wa mjomba wao, hivyo hakuna aliyejua kama nilikuwa nina ujauzito.

Je, kilifuatia nini? Usikose wiki ijayo. Maoni, nicheki kupitia namba hiyo hapo juu.

Leave A Reply