The House of Favourite Newspapers

KINACHOENDELEA MSIBA WA MTOTO WA KIGWANGALLA

Baadhi ya watu wakiwemo mawaziri na Majirani waliojitokeza kwenye msiba mtoto wa Dk. Kigwangalla.

 

MSIBA wa Zulqarinain Mtoto wa Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Andrea Kigwangalla upo nyumbani kwake Mikocheni A katika Kota za Mawaziri jirani na Victoria.

 

Kwa mujibu wa Msemaji wa Familia, Bw. Lumola anataarifu kuwa mwili utasafirishwa kesho asubuhi kwa ndege na Mazishi yanatarajiwa kufanyika saa Kumi jioni Nzega Vijijini Jimboni kwa Waziri Dk Kigwangalla.

Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani Dar es Salaam na Nzega Vijijini. Msiba umetokea leo February 21 majira ya Saa nne asubuhi JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE – MUHIMBILI. Zulqarinain alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo.

Inna lillahi wainna illaihi rajiuun.

Comments are closed.