The House of Favourite Newspapers

Kingwendu Apimwa Ubavu

0

MSANII maarufu wa vichekesho Bongo, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ amepimwa ubavu na mchekeshaji kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Bienvinu Prosper almaarufu Jackson baada ya kufanya naye kazi moja inayokwenda kwa jina la Mkongo Mtata.

 

Kazi hiyo ambayo imekuwa gumzo inapatikana kwenye chaneli ya msanii huyo wa Kongo kwenye Mtandao wa YouTube katika Chaneli ya Beyond Vison TV.

 

Akipiga mastori na IJUMAA SHOWBIZ, Jackson anasema aliamua kufanya kazi na Kingwendu kwa sababu ni mtu ambaye anamvutia na anafurahishwa na kazi zake.

 

“Natamani kufanya kazi na wasanii mbalimbali Bongo, lakini ndoto yangu ya kwanza ilikuwa ni Kingwendu na ndiyo maana tukaachia kazi ya pamoja,” anasema jamaa huyo.

STORI: IMELDA MTEMA

Leave A Reply