The House of Favourite Newspapers

Kinywaji hiki huondoa sumu, kitambi!

0

TIKITIMAJIUondoaji wa sumu mwilini ni muhimu kwa sababu kitendo hicho huondoa mafuta yanayosababisha unene au vitambi. Pia mwili unapokuwa msafi huwezesha mfumo wa chakula kunyonya vizuri virutubisho kutoka kwenye vyakula, pia huondoa chembechembe mbaya zinazosababisha magonjwa ya saratani nk.

ParsleyKwa mujibu wa tafiti za afya, kitambi huweza kuwa dalili moja ya mtu mwenye kisukari aina ya pili (Diabetes Type II). Pia kitambi kina uhusiano na magonjwa ya presha, ya moyo na kwamba kinaweza kusababisha kifo kutokana na mshituko wa moyo.

Hivyo, ili kujiepusha na madhara yatokanayo  na kitambi  na unene wa kupindukia, ni kula lishe bora na kufanya mazoezi mara kwa mara. Aidha, unaweza kutumia lishe maalum kwa kuondoa mafuta ya ziada na sumu mwilini.

CucumbersLeo, tutakujuza kuhusu kinywaji maalum ambacho ni rahisi kutengeneza lakini chenye faida nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na kuondoa sumu, mafuta ya ziada, kung’arisha ngozi, kuboresha mfumo wa kinga, usagaji chakula na kupunguza uzito.

MAHITAJI KWA MTU MMOJA

Tango moja la ukubwa wa wastani, kipande kimoja cha limao, fungu moja la majani ya kotimiri (Parsle), kijiko kimoja kikubwa cha tangawizi mbichi iliyokatwakatwa vipande na maji safi robo tatu ya kikombe.

JINSI YA KUANDAA

Baada ya kukusanya mahitaji hayo na kuhakikisha kila kitu kimeoshwa, vyote pamoja weka kwenye mashine ya kutengeneza juisi (Juicer au Blender). Saga ili kupata juisi. Kipande cha limao utakikamua tu juu ya mchanganyiko huo.

Kwa mahitaji yaliyoainishwa hapo juu, utapata kiasi cha glasi moja ya juisi. Ni vyema ukanywa kila usiku kabla ya kulala na hivyo ndani ya muda mfupi utaweza kuondoa sumu mwilini, kuimarisha kinga ya mwili na wakati huohuo kuondoa kitambi na unene.

Leave A Reply