The House of Favourite Newspapers

Kisa Fumanizi, Mrembo Atimuliwa Kijijini

0

UONGOZI wa kitongoji cha Namayana katika Kijiji cha Namayana wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha, umetoa siku saba kwa mkazi mmoja eneo hilo (Rukia Saidi) kuondoa makazi yake katika kitongoji hicho baada ya kushikwa ugoni akituhumiwa kujihusisha na tabia iliyokubuhu ya kutembea kimapenzi na wanaume za watu.

 

 

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya kufumwa akiwa na mume wa mtu aliyetajwa kwa jina la Richard Ngulwi mkazi wa eneo hilo akibandua amri ya sita nyumbani kwa mwenye mali na kuibua sekeseke la haja lililopelekea kuvunjwa kwa vioo vya madirisha na milango ya mwenye nyumba.

 

 

Akizungumza na vyombo vya habari jijini hapa, Balozi wa nyumba 10 wa kitongoji hicho, Julias Laizer alisema wamelazimika kumfukuza mkazi huyo katika kitongoji chao baada ya kuchoshwa na uchafu wa tabia iliyokithiri ya kutembea na waume za watu kinyume cha sheria.

 

 

Alisema hivi karibuni muda wa saa nane usiku katika kitongoji hicho mtuhumiwa Rukia alifumwa chumbani akiwa na mwanaume aliyetajwa kwa jina la Richard Ngulwi ambaye ni mfanyabiashara wa duka anayedaiwa ni mume wa mwanamke aliyefahamika kwa jina la Margret Raymond.

 

 

Balozi Laizer alisema kuwa baada ya kupata taarifa na kufika eneo la tukio, alimkuta mwanamke aliyedai ni mke wa Richard akiwa nje ya nyumba akiendelea kufanya fujo kwa kuvunja milango na vioo huku mwanaume anayedai ni mume wake akiwa amejifungia ndani “Baada ya kuona hali si shwari niliamua kuripoti tukio hilo polisi na kuwaomba waje.

 

 

Baada ya askari hao kufika waliingia ndani na kumtoa huyo mwanaume lakini mwanamke aliyekuwa naye alikimbia “ alisema Laizer Alisema kesho yake uongozi wa kitongoji hicho ulikutana na kuwaita wahusika ofisini na baadaye maamuzi yalichukuliwa kwa kumpatia mtuhumiwa barua ya kumtimua katika kitongoji hicho ndani ya siku saba.

 

 

Kwa mujibu wa Balozi hiyo Rukia haishi na mwanaume ila anawatoto watatu na hana kazi inayoeleweka ya kumwingizia kipato jambo ambalo wanahisi anawachufulia kitongoji.

 

 

Akizungumzia kadhia hiyo, mfanyabiashara Richard Ngulwi (Richi) alikiri kufumaniwa na mke wake akiwa na mwanamake huyo na kueleza kuwa jambo hilo limetokea kwa bahati mbaya kwa kuwa alikuwa katika hali ya ulevi hakuwa anajitambui.

 

 

“Ni kweli mke wangu alinifuma katika chumba changu nipo na mwanamke mwingine lakini nilikuwa nimelewa pombe sijitambui hata hivyo jambo hilo tumelimaliza “ alisema Richard ambaye huwa haiishi na mke wake, anahisi kuna watu waliomsomea ramani na kumtonya mke wake ambaye naye aliweka mitego yake na kumnasa mgoni wake akivinjari na baba watoto wake kunako sita kwa sita Aliongeza kuwa uharibifu wa nyumba uliofanywa na mkewe tayari amesharekebisha na alimwomba radhi mwenye nyumba kutokana na tukio hilo.

 

 

Kwa upande wa mmiliki wa myumba iliyoharibiwa kwa vioo, Mathias Laizer alisema kuwa akiwa nyumbani kwake amelala majira ya usiku alisikia kelele na kuamka ambapo alikuta vurugu zilizosababisha uharibifu mkubwa wa nyumba yake kuvunjwa kwa vioo na milango.

 

 

Alisema uharibifu huo ulitokana na wivu wa mapenzi ambapo mke wa mpangaji wake alivunja vioo akidai kumfumania mume wake akiwa na mwanamke mwingine Akiongea kwa njia ya simu, mke wa Richard, Margret Raymond alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sasa kwa kuwa ni jambo la aibu. “Nimesema siwezi kuongea chochote kuhusu hilo jambo mtafuteni hiyo mwanamke” alisema na kukata simu.

Stori: Joseph Ngilisho, Arusha

Leave A Reply