The House of Favourite Newspapers

Nandy, Kiba, Utamu Unakuja, Unakata

0

MTOTO mkali kunako gemu ya muziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ hivi karibuni ameachia bonge moja la ngoma iliyokwenda kwa jina la Nibakishie huku akiwa kamshirikisha mfalme wa muziki huo Ali Salehe Kiba ‘Alikiba’ jambo lililozua tafrani mitandaoni na kufanya utamu wa wasanii hao kimahaba kuja na kukata kiaina.

 

Wimbo huo ambao uliachiwa mapema wiki hii ulionekana kuwavutia wengi na kutrendi vilivyo mjini YouTube lakini vipande tata vya video yake ndiyo iliyokuwa habari ya mjini huku wengi wakidai kuwa huwenda wawili hao wamefika mbali zaidi ya kinachoonekana kwenye video.

 

Machezo aliyofanya Nandy na Alikiba kwenye video hiyo yaliwafanya wengi waingiwe na ‘pepo mchafu’ huku wengine wakisema “mbona iko poa tu.”

 

“Mmmh! Jamani hapana hii video inashawawishi sana, sidhani kama Nandy alitoka salama hapa, lazima kuna kitu kilifanyika,” alikomenti mtu mmoja kwenye ukurasa wa Instagram ulioposti kipande cha video ya wimbo huo.

 

Mwingine aliandika: “Haya mahaba wanayoonyeshana kwenye hii video ni balaa tupu, walahi ingekuwa mimi ndio Billnass (mchumba wa Nandy) ningefanya juu chini nimpate Amina (mke wa Kiba) halafu nirekodi naye video kama hii ili tuwe na maumivu sawa.”

 

Aliyefuata akatupia maneno yake hivi:

“Kuolewa na msanii inataka moyo sana, unatakiwa ukae na vidonge vya presha wakati wote,” baada ya maneno hayo akasindikiza na emoj za kulia.

Utamu mwingine wa komenti kutoka kwa mashabiki wengine ulikuwa ni huu:

“Dah kwa staili hii bi Amina ndiyo asinune jamani.”

 

“Nimeangalia video nzima sijaona kitu kinachowafanya Watanzania wengi wajaji, kwa sababu ni kazi na wao wapo kazini hivyo ni lazima waonyeshe uhalisia.”

Aidha komenti zilizidi kutiririka kama mvua kwenye video hiyo na kuleta mjadala mzito miongoni mwa watu.

Kufuatia kelele hizo mwandishi wetu alimvutia waya Alikiba na kumuuliza akiwa kama mume wa mtu vipi video hiyo haikuchachua ndoa yake?

 

“Sanaa yetu ina mambo mengi sana, ili ufikishe ujumbe kwa jamii lazima uelimishe na kuburudisha watu, mimi mke wangu ananisapoti na anaona, anaelewa.

“Lakini pia ni kawaida kwa mwanamke kusikia wivu, kukasirishwa na vitu kama hivyo, lakini mwisho wa siku hiyo hali inapita anaelewa.

“Hata kwa Billnass yeye alikuwepo wakati tunafanya video hiyo anamsapoti Nandy na anaelewa kwa sababu yeye pia ni msanii.

“Japo kwa mwanamke kidogo ni kazi lakini Billnass nadhani anaelewa, pia heshima ambayo nipo nayo kwao ni kubwa sana.

“Kwa hiyo watu wasifikirie kama kuna chochote kinachoendelea kati yetu, ni kazi tu,” alisema Alikiba.

Hayo ni maneno ya Alikiba, kwamba “ni kazi tu”, mengine ya utamu kati yao unakuja, unakata ni ya mitandaoni.

 Stori: Memorise Richard, Dar

Leave A Reply