The House of Favourite Newspapers

Kisa kuuza maneno, washkaji hawa wanaishi kishua usipime

0

50cent.jpg50 Cent.

Makala: Boniphace Ngumije

“Asante Mungu kwa kipaji.” Ni kauli ambayo Mwanamuziki wa Hip Hop mwenye jina kubwa duniani 50 Cent kupitia kipindi cha runinga fulani Marekani kiitwacho The Breakfast Club aliwahi kueleza kuwa kila anapoamka hata kama hana mpango wa dili anaoufikiria lazima aitamke.

50 Cent alimaanisha kipaji ni kila kitu kwenye maisha yake na kwa kuwa anakipaji ameweza kupata mambo mengi aliyotamani kuwa nayo maishani. Hivyo ndivyo ilivyo kwa washkaji hawa ambao wanauza maneno (kuchekesha) na kuingiza mkwanja kuliko kawaida.

masanja2Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’

Kwa upande wa Bongo, miongoni mwa wachekeshaji wachache waliovuna mafanikio makubwa ni Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’  ambaye anamiliki nyumba za kishua tatu Bongo, kampuni ya ulinzi, mashamba kibao ya mpunga na magari zaidi ya matano ya bei mbaya.

omondEric Omondi

Ukiachana na Masanja na kuvuka mpaka kidogo tu na kutua nchini Kenya unakutana na mshkaji ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika tasnia hiyo Afrika Mashariki, Eric Omondi. Huyu jamaa ni noma na milionea, unaambiwa kupitia ushereheshaji kwenye matamasha, matangazo, kuchekesha majukwaani, utajiri wake kwa sasa unakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 640 za Kitanzania.

Anne KansiimeAnne Kansiime.

Pasipo kwenda mbali tukiwatembelea jirani zetu Waganda tunamkuta Malkia wa Komedi Afrika, Anne Kansiime. Mwanadada huyu ni mshindi wa tuzo nyingi za komedi Afrika kupitia utitiri wa video zake katika Mtandao wa Kijamii wa YouTube zinazotazamwa na zaidi ya watu milioni 15.  Si muwazi sana katika kuanika mali zake lakini kupitia matangazo ya kibiashara ya ‘local’ na yale ya kimataifa, kipindi cha televisheni kinachorushwa na Go Tv ya Uganda pamoja na kazi yake ya kuchekesha anaingiza mkwanja mrefu unaomfanya kuishi kishua usipime.

Ayo Makun ‘AY’Ayo Makun ‘AY’

Ayo Makun ‘AY’ au maarufu Nigeria kwa jina la Masta wa Sanaa ni miongoni mwa wasanii vijana wenye mafanikio makubwa Afrika. Kwa Nigeria si wa kwanza yupo nyuma ya kina Julius Agwu, I Go Dye na Ali Baba lakini umri wake wa miaka 38 kwa sasa unamfanya kukaa katika orodha hii akiwa kijana na tajiri. Utajiri wake kupitia michongo mbalimbali kama walivyo komediani wengine hapo juu unakadiriwa kuzidi milioni 800 za madafu.

Leave A Reply