The House of Favourite Newspapers

Kisa Mabao, Okwi Ahamishia Mke Ghorofani

Emmanuel Okwi.

STRAIKA wa Simba, Emmanuel Okwi amemleta mkewe na familia yake Jijini Dar es Salaam na watakuwa wakiishi kwenye ghorofa la kifahari maeneo ya Upanga chini ya ulinzi mkali.

 

Okwi alisema kuwa amelazimika kumleta mke na wanae ili aweze kupata muda wa kuitumikia Simba bila kuwa na mawazo ya familia hiyo ambapo awali alikuwa akiifikiria sana kutokana na kuwa mbali nayo.

“Nipo na mke wangu na ataen-delea kuwepo kwani lengo ni kuwa nae karibu ili tuweze kusapotiana kwa kila kitu maana uwepo wake unanifanya kupata utulivu kwenye kazi yangu, hivyohivyo hata yeye anakuwa na furaha kwa kuwa muda wote tupo pamoja,” alisema mchezaji huyo kipenzi cha mashabiki wa Simba.

“Wazo langu kubwa kwa sasa ni kuangalia namna gani nitaipambania timu, lakini nami kujitengenezea mazingira mazuri kwa kuifungia.”

Comments are closed.