The House of Favourite Newspapers

Heritier Makambo: Nipanieni Niwalize

 

MSHAMBULIAJI tegemeo wa Yanga Mkongomani, Heritier Makambo amewaambia mabeki wa timu pinzani waendelee kumchezea kwa kum pania, lakini atafunga tu mabao.

 

“Siku zote hakuna beki anayekubali kupitwa kirahisi na mshambuliaji na kwenda kufunga bao, ni lazima beki apambane kukuzuia wewe mshambuliaji ili usifunge.

 

“Hivyo, kwangu sioni cha ajabu kuona mabeki hao wakija uwanjani kwa ajili ya kunifuata kunizuia zaidi ninajipanga kuhakikisha ninakabiliana nao kuifungia timu yangu mabao,” alisema Makambo.

Kocha na Ajibu

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa; “Ajibu ambaye nilikuwa natamani kumuona kwa sasa nimeanza kumuona ingawa kwa sasa nahitaji yeye apambane atengeneza nafasi nyingi za kufunga na hata yeye mwenyewe aweze kufunga na aweze kusaidia timu.”

 

“Siku zote nasema Ajibu mchezaji mzuri ila kuna vitu ambavyo anahitaji kuvifanyia kazi sana na kwa umakini mkubwa na akifanikiwa hapo basi tutakuwa tunazungumza habari nyingine zaidi aongeze bidii na kufanya mazoezi,”alisema Zahera.

 

Ajibu mwenyewe aliongeza kwamba; “Kikubwa ambacho kimechangia mafanikio haya ndani ya timu ni ushirikiano uliopo ndani ya timu kwani ushindi ni wa timu, mipango inayoendelea ni kuhakikisha kwamba naendelea kufanya vizuri kwa ajili ya mechi zingine ambazo zinakuja mbele yangu bila kujali nacheza na nani kwetu sisi kitu muhimu ni pointi tatu.”

Comments are closed.