The House of Favourite Newspapers

KISUTU: Kesi ya Nyerere Yapigwa Kalenda Tena

0
Yeriko Nyerere akitoka nje ya lango la Mahakama ya Kisutu.

 

KESI inayomkabiri mfanyabiashara, Yeriko Nyerere ya makosa ya uchochezi wa njia ya mtandao imeahirishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam hadi Agosti 22 mwaka huu.

 

Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu, Wilbard Mashauri kutokana na kile alichosema Wakili wa serikali, Elia Atanas anayeisikiliza kesi hiyo, kutokuwepo mahakamani kwa sababu alipata ajari.

 

Yeriko anakabiliwa na mashtaka matano ya kutoa taarifa za upotoshaji kwa njia ya mtandao ambapo kesi hiyo ilitakiwa kusikilizwa ushahidi leo.

Katika kesi hiyo mawakili wanaomtetea mshitakiwa ni Tundu Lisu na Peter Kibatala.

 

LIVE: Ziara ya Waziri wa Utumishi, Angellah Kairuki Wilaya za Mkoa wa Dar

Leave A Reply