The House of Favourite Newspapers

Kitenge Aondoka Wasafi, Arejea EFM

0

Uongozi wa Wasafi Media umetangaza mtangazaji wake maarufu, Maulid Kitenge anaondoka katika kituo hicho. Mkurugenzi wa Wasafi, Diamond Platinum amemshukuru kwa mchango wake alioutoa na kumtakia kila la kheri. Kitenge alijiunga na Wasafi akitokea Redio ya EFM na sasa amerejea tena EFM.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram CEO wa EFM, Majizzo ameandika; “Tarehe 18 Octoba 2019, nilipost hapa ‘instagram’ kumuaga ndugu #MaulidKitenge ikiwa ni baada ya kukaa naye kwa takriban miaka 5. Mimi na yeye tuliagana vizuri, tulitakiana heri. Tuliachana kwa wema. Kwangu maisha yanapaswa kuwa hivyo.

 

“Baada kukamilisha yaliyompeleka kule #KochaMchezaji Maulid Kitenge, anarudi tena hapa ambapo bila shaka ni nyumbani kwake. Yeye ni kati ya watangazaji wa mwanzo hapa EFM, ni furaha kubwa sana kumkaribisha tena tufurahie pamoja hatua tulizofikia na kuendeleza mapambano zaidi.

Leave A Reply