The House of Favourite Newspapers

LIVE KUTOKA TEGETA: Kituo cha Mafuta Chanusurika Kuteketea kwa Moto

Kituo cha mafuta cha Petro kilichopo Tegeta Azania jijini Dar es Salaam, kimenusurika kuteketea kwa moto baada ya gari la kubebea mafuta lililokuwa likipakua shehena ya mafuta kituoni hapo, kupata hitilafu na kushika moto kisha kuteketea lote.

Moto huo mkubwa ulisababisha  barabara kufungwa kwa muda, na kusababisha kukosekana kwa mawasiliano kati ya pande hizo mbili, ambapo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na makampuni binafsi ya zimamoto, walifanikiwa kuuzimamoto huo.


Shukrani za kipekee zimuendelee dereva wa gari lililoshika moto, Edwin Thomas ambaye kwa ujasiri mkubwa aliweza kuingia ndani ya gari baada ya kuona limeshika moto, akalisogeza kutokakwenye visima vya mafuta lilipokuwepo mpaka pembeni kabisa, ambapo moto ulipomzidi alishuka kwenye gari lakini akiwa tayari ameshaliondoa kwenye visima vya mafuta.

 

Comments are closed.