The House of Favourite Newspapers

KMKM Waendelea na Zoezi la Uokoaji Pemba

0

ZOEZI la uokoaji na kutafuta miili, linaendelea kisiwani Pemba kufuatia kuzama kwa boti iliyokuwa inatokea Chakechake kuelekea katika Kisiwa cha Panza na kusababisha vifo vya takribani watu tisa huku wengine kadhaa wakiokolewa.

 

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Matar Zahor Masoud amesema ajali hiyo ilitokea jana Jumanne Januari 4, 2022 jioni na kwamba askari wa Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) kwa kushirikiana na wananchi, walifanya zoezi la uokoaji hapo jana lakini kutokana na giza kuingia na bahari kuchafuka, walisitisha zoezi hilo na kuendelea leo asubuhi.

 

Maiti zilizookolewa pamoja na majeruhi, wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoani ambapo mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kutoa ushirikiano na kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu.

Leave A Reply