The House of Favourite Newspapers

Wema Sepetu Amvaa Shabiki Kisa Kuzaa

0

MALKIA wa Bongo Muvi, Wema Sepetu amejikuta akishindwa kuvumulia na kuamua kumtolea makavu bila chenga shabiki aneyafahamika kwa jina la Lukondej baada ya shabiki huyo kukoment kwenye  post ya Wema aliyoweka akiwa na mtoto inayesemekana ni wa dada yake.

 

Wema alipost picha akiwa na mtoto huyo kisha akasema; ‘‘My heart, What you see is what you get.’’ baada ya kuweka post hiyo, shabiki huyo alikuja na kukomenti maneno haya “Zaa wa kwako ndio utuulize swali bwana wee.” Kitendo hiki kilionekana kumuuma Wema aliyeshindwa kuvumilia na kujikuta akiandika maneno mazito.

 

Wema alifunguka kwa kusema kuwa “Sikieni, kila siku kuniambia nizae wangu, unadhani staki au? Nataka ten asana, sijui unanielewa? Je kama siwezi zaa?nataka mtoto sana. Kuna muda mpaka nashindwa kupost picha ya mtoto just cause I know mtaniattack,” alisema Wema.

 

Mashabiki mbalimbali wa Wema walijitokeza kumuombea staa huyo abarikiwe kupata mtoto kama mastaa wenzie huku wengine wakilaani kauli ya shabiki huyo kwa kusema hupaswi kumcheka mtu kuhusu mtoto, ndoa na kipato kwa sababu Mungu pekee ndiye anayejua.

 

Wema ambaye ni Mshindi wa taji la urembo Tanzania (Miss Tanzania 2006), kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuitwa mama (kupata mtoto) kama mastaa wengine wanavyoitwa kama vile kina Aunty Ezekiel, Kajala na wengine wengi waliobarikiwa kupata watoto lakini kwake imekuwa ni mtihani.

 

Mnamo Mei, mwaka 2021 , Wema alitikisa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kufuatia kauli yake kwa staa mwenzie Jackline Wolper aliyebarikiwa kupata mtoto mwaka huo. Wema alipost katika akaunti yake ya Instagram akimpongeza Wolper kwa kupata mtoto huku akionekana kuwa mtu mwenye huzuni kwa kubaki pekee yake kupata mtoto huku mastaa wenzie wakiendelea kuitwa mama.

 

Mbali na hilo, Septemba 2021 pia baada ya Vanessa Mdee kupata mtoto na staa kutoka Marekani Rotimi, Wema Sepetu alipost katika akaunti yake ya Instagram akimpongeza staa huyo huku akisema anamuonea wivu Vanessa Mdee kwa kupata mtoto.

Leave A Reply